Monday, December 1, 2014

Aliyempiga Messi kupigwa kifungo cha maisha


Valencia wamesema watamfungia maisha shabiki aliyempiga na chupa ya plastic mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi katika mchezo wao wa jana wa la liga.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 27 alikuwa akishangilia na wenzake bao lilifungwa na Sergio Busquets wakati alipopigwa na chupa hiyo.

Messi hakuumia katika tukio hilo lakini Valencia katika taarifa yake imesikitishwa na kulaani tukio hilo.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa klabu hiyo itafanya juhudi kuhakikisha shabiki huyo anakamatwa na kuchukuliwa hatua na atafungiwa maisha kukanyaga Mestalla.

Kocha wa Barcelona Luis Enrique amesema klabu za Hispania zinapigania kuondoka kwa vitendo hivyo vya mashabiki wanaoleta vurugu michezoni.

Mapema katika siku hiyo ya jana shabiki amefariki baada ya kutokea vurugu baina mashabiki kabla ya mchezo wa nyumbani wa Atletico Madrid dhidi ya Deportivo La Coruna.

Thierry Henry huyoooo Arsenal,aitema rasmi New York Red Bulls


Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry ameitema timu ya New York Red Bulls baada ya kuitumikia kwa miaka minne na nusu kuna ligi kuu ya nchini Marekani MLS.

Mechi ya mwisho kwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 37 ilikuwa ni walipotoka sare ya kufungana mabao 2-2 Jumamosi iliyopita hiyo ikiwa na maana Red Bulls wameondolewa kwa jumla ya mabao 4-3 na New England Revolution katika mechi za mtoano za ubingwa wa Eastern Conference.

Henry mwenyewe anasema maamuzi yake tokea awali ilikuwa ni kuondoka baada ya kumaliza muda wake wa mkataba.

Amesema itamchukua wiki chache zijazo kuamua hatima yake ya baadaye.

Hata hivyo taarifa zinasema kuwa Henry anarejea Arsenal katika benchi la ufundi ili kuongeza nguvu kwa washika bunduki hao.