Wednesday, August 7, 2013

Barcelona yagonga hodi Chelsea,yamtaka Luiz


Barcelona wamegonga hodi kwa Chelsea kumtaka beki David Luiz.

Wakali hao wa Hispania wamehusishwa kwa muda mrefu kumtaka beki huyo lakini sasa si stori tena wameingia rasmi.

Lakini kocha wa The Blues Jose Mourinho amesisitiza kuwa beki huyo mwenye miaka 26 haendi kokote kwakuwa bado yumo kwenye mipango yake.

Mourinho amesema Luiz bado anatakiwa na ubora wake bado unahitajika darajani.

 
Luiz amesaini mkataba mpya wa miaka mitano na Chelsea September mwaka jana na amecheza zaidi ya mechi 100 tokea amejiunga akitokea Benfica January 2011.

Alihusishwa na kutaka kutimkia Manchester United ikiwa ni sehemu ya mpango wa kumnasa mshambuliaji Wayne Rooney mpango ambao ulikanushwa haraka na Chelsea.

Pia alihusishwa kutakiwa na Bayern Munich inayofundishwa na kocha wa zamanin wa Barcelona Pep Guardiola. 




Lakini Guardiola,akizungumza wiki iliyopita kabla ya kombe la Audi huko Munich alisema anafurahia chaguo la sehemu ya ulinzi alilokuwa nalo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.